Wakaazi wa Kuresoi Kusini Wanufaika na Maji Safi Kupitia Mradi Mpya


Kuresoi Kusini: Wakaazi zaidi ya 1,500 kutoka wadi ya Keringet katika eneo bunge la Kuresoi Kusini wanatarajiwa kunufaika na maji safi ya kunywa yatakayoletwa na mradi wa maji wa Soitaran ambao unapangwa kuanza wiki hii. Mradi huu wa maji, unaoendeshwa na Serikali ya Kaunti ya Nakuru, unanuiwa kuhakikisha kuwa wakaazi wanatumia maji safi nyumbani mwao na pia kwa maslahi ya ufugaji; hali ambayo itawawezesha kujiepusha na maradhi yanayosababishwa kwa kutumia maji machafu.



According to Kenya News Agency, Afisa wa Maji wa eneo hilo, James Tirop, amesema maji ni muhimu sana katika maisha ya binadamu na hivyo basi akawaomba wakaazi kuitumia rasilimali hii vyema pindi tu mradi huu utakapokamilika ili kuwanufaisha muda mrefu. Aidha aliongeza kwamba wakaazi watapata muda wa kushughulikia mambo mengine kwa kuwa wako na maji safi manyumbani mwao kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo walitembea kilomita tatu ili kuchota maji safi.



Baadhi ya vijiji vitakavyonufaika na mradi huu ni kama vile Lelaibei, Soitaran, Tabaita na Sigowet. Tirop aliwahakikishia wakaazi kuwa watapewa kipao mbele katika kupewa vibarua wakati mradi huu unaendelea kujengwa na hivyo basi kuwasihi kutumia mapato yao vizuri ili kujinufaisha. Usambazaji wa maji masafi ni nguzo kuu katika ahadi za Gavana Susan Kihika ambaye kufikia sasa, kupitia idara ya maji ya kaunti, kumechimbwa visima 66 huku 52 vikiwa visima vitumiavyo nguvu za jua.

Latest post